HAKI YA MAANDAMANO NA MIKUSANYIKO
TANZANIA
Utangulizi
Haki ya kuundamana na kukusanyika ni haki za
msingi kwa kila mtu, hizi ni haki ambazo zimeruuhusiwa kwa mujibu wa sharia za
ndani Pamoja na sharia za kimataifa ambazo Tanzania imezisaini. Miongoni mwa
sharia hizo za kimataifa ni Tamko la kimataifa la haki za
binadamu la mwaka [1948], Mkataba wa kiafrika wa haki za binadamu na haki za
watu wa mwaka [1981], na mkataba wa haki za kisiasa na kiraia wa
mwaka [1966] kwa mujibu wa sharia za ndani ni Pamoja na
sharia mama ya nchi ambayo ni katiba ya jamhuri ya muungano wa
Tanzania ya mwaka [1977] sura ya pili .
Katika ukurusa ntaenda kueleza uhalali wa haki hizi yaani haki ya
kukusanyika Pamoja na haki ya kuundamana na utaratibu wa kuzitekeleza kwa mujibu wa sharia za nchi ya
jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Uhalali wa maandamano na mikusanyiko
Tanzania
Haki ya kuandamana na kukusanyika
hizi miongoni mwa haki za msingi kwa binadamu kama jinsi zilivyo haki zingine,
hizi ni haki ambazo zinauhusiana na haki za kisiasa na kiraia. Mikusanyiko na
maandamo ni sehemu muhimu kwa binadamu katika kuelezea mtazamo wake au kutoa
maoni yake au kupinga jambo Fulani pia inaweza kuwa kuunga mkono jambo Fulani
na mengineyo mengi.
Kwa mujibu wa katiba ya nchi yaani
naamanisha sharia mama ya Tanzania [katiba ya jamhuri ya
muungano wa Tanzania ya mwaka [1977] sura ya pili Ibara ya (20) ibara ndogo ya kwanza (1) ambayo imempa kila mtu
haki ya kufanya maandamano Pamoja na haki ya kukusanyika, kwa lengo la kueleza
mawazo yao au kutoa maoni yao
hadharani. Sitotaka kuelezea sana katika
hili kwa sababu sharia yenyewe iko wazi kabisa ukerejelea kwenye katiba ya
Tanzania sehemu ya tatu kwenye [BASIC RIGHT AND DUTIES] ibara ya (20) ibara
ndogo ya kwanza imeeleza wazi kabisa na wala hilo halina ubishi kuwa kila mtu
ana haki ya kuundamana Pamoja na kufanya mikusnayiko ili kuelezea maoni yao
hadharani.
Mpaka hapo nadhani tutakuwa tumeafikiana kuwa haki ya kuundamana na kufanya mikusamyiko ni haki halali kabisa kwa mujibu wa katiba ya nchi na sitotaka kuzichambua sharia zingine za nchi juu ya uhalali wa haki hizi kwa sababu kwa sababu katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 sura ya pili ndio sharia mama wa sharia zote na ndio sharia kuu na sharia yeyote itakayo pingana na katiba basi hiyo sharia ni batiri kwa mujibi wa ibara ya (64) ibara ndogo ya (5).
Utaratibu wa kufanya maandamano na mikusanyiko kisheria
Katika kipengele hichi naomba uwe makini unapo kisoma, ikotokea
kuna chama au taasisi au mtu anataka kufanya maandamano au mikusanyiko sehemu
ya umma, kwa mujibu wa sharia anatakiwa kutoa taarifa (notification) ya
maandishi kwa jeshi la polisi angalau masaa 48hrs kabla ya mikusanyiko au
maandamano yanayo kusudiwa kufanyika. Katika taarifa inatakiwa ieleze mahala
ambapo maandamano hayo yanakusudiwa kufanyika, muda wa maandamano au mkusanyiko
huo utafanyika pia inatakiwa kwenye taarifa hiyo ieleze lengo au kusudio la
maandamano hayo au mkusanyiko.
Na hapa naomba nieleweke vizuri, taasisi au chama au mtu itatakiwa
kutoa taarifa juu ya mkusanyiko huu au maandamano hayo kwa jeshi la polisi
iwapo yatakuwa yanakwenda au yatafanyika katika eneo la umma kama
hayatakusudiwa kufanyika eneo la umma baasi hakuna taarifa yeyote itatolewa na
ieleweke kuwa hapa inayo tolewa TAARIFA tu ni siyo maombi
Kwaiyo ni muhimu ikaeleweka kuwa jeshi la polisi halina maamlaka
juu ya uamuzi wa mikusanyiko au maandamano kama lingekuwa na maamlaka basi
sharia ingeemka anayeteka kufanya maandamano afanye maombi (application) lakini
badala yake linamtaka mkusudiwa kutoa notification (taarifa)
Maamlaka ya waziri wa mambo ya ndani juu haki ya mikusanyiko na maandamano Tanzania
Waziri wa mambo ya ndani ana maamlaka makubwa haswa kwenye maswala
ya kuundamana na kukusanyika. Waziri amepewe uwezo wa kuongeza vigezo ambayo
mtu anatakiwa kuivyipelek polisi kabla ya kufanya mikusanyiko au maandamano.
Na ikitokea mtu hajaridhishwa na maamuzi yaliyo tolewa na polisi
anatakiwa akate rufaa kwa waziri wa mambo ya ndani na maamuzi yatakayo tolewa
na waziri wa mambo ya ndani ndio maamuzi ya mwisho na wala hayana rufaa.
Pia waziri wa mambo ya ndani amepewa maamlaka ya kuamurukuwa mkusanyiko au maanadamano yeyote yasifuate sharia na taratibu zinahusu mikusanyiko au maandamano na mtu anayeanda maandamo hayo au mkusanyiko huu atakuwa ametenda kosa la jinai
Maoni yangu juu ya maamlaka ya waziri wa mambo ya ndani kuuhusu
mikusanyiko na maandamano
Katika mfumo wetu wa Tanzania wazari mambo ya ndani anakuwa ni
mwanasiasa wa chama tawala kwaiyo kitendo cha yeye kupewa maamlaka ya kuongeza
vigezo anaweza kuongeza vigezo ambavyo vitakuwa vigumu kwa mpinzani wake pia
kuamuru mkusanyiko au maandamo ya chama chake au taasisi aliyo na mslahi nayo
yafanyike , pia ukiangalia waziri wa mambo ya ndani amepewe maamlaka ya rufani
pale inapo tokea mtu hajaridhishwa na maamuzi yaliyo tolewa na chombo cha
polisi pia katika hili limetoa mwanya wa ukandamizaji ikitokea mrufani ni
mpinzani wa waziri wa mambo ya ndani, yaani kikubwa Zaidi maauuzi ya waziri
ndio yatakuwa ya mwisho na wala hayana ruufa, ambapo kwa taswira ya Mahakama
inapinga vipengele ambavyo vinapinga jambo kutokufika mahakamani, katika
mtizamo wa mahakama inataka ikotokea mtu haridhishwa na maamuzi yaliyo tolewa
na chombo chochote cha uongozi kwenda mahakama kuu kuomba marejeo ya uuamuzi.
Mwisho kabisa naona sharia ingaemtaka wazi waziri ni aina gani ya
maadamanona mikusanyiko amabayo inaweza isifuate sharia kuliko kumuachia waziri
mamlaka makubwa ya kuuamua ni mikusanyiko na maandamano gani yasifuate taratibu za kisheria, katika utawala wa
kisheria unataka kufanya kazi kwa kufata usawa, amapo ukirejere katika ibara ya
(13) ibara ndogo ya kwanza ya katiba ya jamhuri wa muungano wa taanzania yam waka
1977 sura ya pili ambayo inamtaka kila mtu kuwa sawa mbele pasipo kuwepo na ubaguzi wa aina yeyote ile
kulindw, kwaiyo mpaka hapo maamlaka aliyo pewa waziri hayako sawa na katiba.
email; jeyma2maduwa@gmail.com
phone no; (255) 0746804719
follow me on ; Facebook@ hd jeyma maduwa
Instagram@ hd jeyma maduwa
twitter@ hd jeyma maduwa (rightmndedpason)
🤝
ReplyDelete