Sunday, June 29, 2025

Mabadiliko ya Sera na Sheria za Uteuzi wa Viongozi na Wagombea wa Nafasi za Uongozi


Elimu na Uongozi: Hoja ya Mabadiliko

✍️ HD Jeyma Maduwa

LL.B. (Hons)

Katika zama hizi za maendeleo ya kasi duniani sayansi, teknolojia, uchumi wa kidigitali na mabadiliko ya kijamii  hatuwezi tena kuamini kuwa kujua kusoma na kuandika pekee kunatosha kumfanya mtu kuwa kiongozi. Uongozi ni zaidi ya uwezo wa kuandika jina lako au kusoma hotuba. Unahitaji maarifa, maono, busara, na weledi wa hali ya juu.

Leo hii, bado tunaona nafasi muhimu za kiuongozi zikishikiliwa na watu wasiokuwa na msingi wa elimu. Je, tunaweza kweli kutarajia mageuzi ya maana katika uchumi, siasa au jamii ikiwa viongozi wetu hawana uelewa wa masuala haya? Viongozi wasio na elimu hawawezi kuelewa changamoto zinazokikabili kizazi cha sasa, wala hawawezi kutunga sera bora au kufanya maamuzi sahihi kwa manufaa ya wananchi.

Kadri tunavyoelekea kwenye uchaguzi mkuu, majina ya watu wanaochukua fomu yanatoa taswira halisi ya hali ilivyo. Kwa masikitiko makubwa, vigezo vya msingi kama elimu, uzoefu au maono hayazingatiwi ipasavyo. Tunashuhudia nafasi za uongozi zikitafutwa kwa kutumia umaarufu wa kisanii, ushabiki wa kisiasa au hata ushawishi wa kifamilia. Hali hii ni hatari kwa mustakabali wa taifa letu.

Na kwa huzuni zaidi, umaarufu umegeuzwa kuwa tiketi ya kisiasa. Mtu akiwa maarufu, hata kama hana mchango wa moja kwa moja kwa jamii, hupewa heshima ya kugombea nafasi nyeti. Umaarufu bila maarifa ni sawa na upofu wa kisiasa. Tusikubali uongozi kuwa ajira ya kawaida au zawadi ya majina makubwa; uongozi ni dhamana inayohitaji ukomavu wa kiakili, elimu, na maadili ya hali ya juu.

Kwa mfumo wa sasa wa sheria, ambapo hakuna masharti madhubuti ya elimu kwa wagombea wa baadhi ya nafasi, tutaendelea kuongozwa kwa kubahatisha. Tutaendelea kulalamika, na mzunguko wa viongozi wasio na dira utaendelea kutugharimu maendeleo yetu kama taifa.

Ni kweli kwamba kujua kusoma na kuandika ni msingi, lakini hiyo haitoshi kabisa. Taifa linahitaji viongozi walioelimika, wenye uelewa mpana wa muktadha wa kisiasa, kijamii na kiuchumi. Uongozi usichukuliwe kama kazi ya kawaida bali kama wito wa kweli wa huduma kwa wananchi. Kiongozi wa kweli ni yule anayebeba maono ya maendeleo na anayejua anapoelekea.

Elimu ni dira. Ni silaha dhidi ya ujinga na upofu wa kiuamuzi. Taifa lolote linalothamini maendeleo lazima liweke elimu mbele — si kwa wananchi tu, bali pia kwa viongozi wake. Uongozi si urithi wa kifamilia wala tuzo ya kisiasa. Ni wajibu unaohitaji maandalizi makini na mwelekeo wa dhati.

Ni wakati wa kufanya mabadiliko ya kisheria. Sheria yetu ihakikishe kuwa wagombea wa nafasi za uongozi wana kiwango cha chini cha elimu kinachowapa uwezo wa kuongoza kwa ufanisi. Tusipochukua hatua sasa, tutazidi kuona taifa likiongozwa pasipo dira, na matokeo yake ni taifa lisiloelekea popote salama.

Uongozi usio na elimu ni sawa na jahazi lisilo na nahodha hatuwezi kufika salama.

#MaarifaKwanza #UongoziBora #ElimuNdiyoNguzo



Monday, September 21, 2020

 

HAKI YA MAANDAMANO NA MIKUSANYIKO TANZANIA


                          JUMA, JUMA MADUWA [hdjeymamaduwa]


 Utangulizi

 Haki ya kuundamana na kukusanyika ni haki za msingi kwa kila mtu, hizi ni haki ambazo zimeruuhusiwa kwa mujibu wa sharia za ndani Pamoja na sharia za kimataifa ambazo Tanzania imezisaini. Miongoni mwa sharia hizo za kimataifa ni Tamko la kimataifa la haki za binadamu la mwaka [1948], Mkataba wa kiafrika wa haki za binadamu na haki za watu wa mwaka  [1981], na mkataba wa haki za kisiasa na kiraia wa mwaka [1966]  kwa mujibu wa sharia za ndani ni Pamoja na sharia mama ya nchi ambayo ni katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania  ya mwaka [1977] sura ya pili .

Katika ukurusa ntaenda kueleza uhalali wa haki hizi yaani haki ya kukusanyika Pamoja na haki ya kuundamana na utaratibu wa kuzitekeleza kwa mujibu wa sharia za nchi ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.



Uhalali wa maandamano na mikusanyiko Tanzania

Haki ya kuandamana na kukusanyika hizi miongoni mwa haki za msingi kwa binadamu kama jinsi zilivyo haki zingine, hizi ni haki ambazo zinauhusiana na haki za kisiasa na kiraia. Mikusanyiko na maandamo ni sehemu muhimu kwa binadamu katika kuelezea mtazamo wake au kutoa maoni yake au kupinga jambo Fulani pia inaweza kuwa kuunga mkono jambo Fulani na mengineyo mengi.

Kwa mujibu wa katiba ya nchi yaani naamanisha sharia mama ya Tanzania [katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka [1977] sura ya pili Ibara ya (20) ibara ndogo ya kwanza (1) ambayo imempa kila mtu haki ya kufanya maandamano Pamoja na haki ya kukusanyika, kwa lengo la kueleza mawazo yao au kutoa maoni   yao hadharani.  Sitotaka kuelezea sana katika hili kwa sababu sharia yenyewe iko wazi kabisa ukerejelea kwenye katiba ya Tanzania sehemu ya tatu kwenye [BASIC RIGHT AND DUTIES] ibara ya (20) ibara ndogo ya kwanza imeeleza wazi kabisa na wala hilo halina ubishi kuwa kila mtu ana haki ya kuundamana Pamoja na kufanya mikusnayiko ili kuelezea maoni yao hadharani.

Mpaka hapo nadhani tutakuwa tumeafikiana kuwa haki ya kuundamana na kufanya mikusamyiko ni haki halali kabisa kwa mujibu wa katiba ya nchi na sitotaka kuzichambua sharia zingine za nchi juu ya uhalali wa haki hizi  kwa sababu kwa sababu katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 sura ya pili ndio sharia mama wa sharia zote na ndio sharia kuu na sharia yeyote itakayo pingana na katiba basi hiyo sharia ni batiri kwa mujibi wa ibara ya  (64) ibara ndogo ya (5).

Utaratibu wa kufanya maandamano na mikusanyiko kisheria

Katika kipengele hichi naomba uwe makini unapo kisoma, ikotokea kuna chama au taasisi au mtu anataka kufanya maandamano au mikusanyiko sehemu ya umma, kwa mujibu wa sharia anatakiwa kutoa taarifa (notification) ya maandishi kwa jeshi la polisi angalau masaa 48hrs kabla ya mikusanyiko au maandamano yanayo kusudiwa kufanyika. Katika taarifa inatakiwa ieleze mahala ambapo maandamano hayo yanakusudiwa kufanyika, muda wa maandamano au mkusanyiko huo utafanyika pia inatakiwa kwenye taarifa hiyo ieleze lengo au kusudio la maandamano hayo au mkusanyiko.

Na hapa naomba nieleweke vizuri, taasisi au chama au mtu itatakiwa kutoa taarifa juu ya mkusanyiko huu au maandamano hayo kwa jeshi la polisi iwapo yatakuwa yanakwenda au yatafanyika katika eneo la umma kama hayatakusudiwa kufanyika eneo la umma baasi hakuna taarifa yeyote itatolewa na ieleweke kuwa hapa inayo tolewa TAARIFA tu ni siyo maombi

Kwaiyo ni muhimu ikaeleweka kuwa jeshi la polisi halina maamlaka juu ya uamuzi wa mikusanyiko au maandamano kama lingekuwa na maamlaka basi sharia ingeemka anayeteka kufanya maandamano afanye maombi (application) lakini badala yake linamtaka mkusudiwa kutoa notification (taarifa)

Maamlaka ya waziri wa mambo ya ndani  juu haki ya mikusanyiko na maandamano Tanzania

Waziri wa mambo ya ndani ana maamlaka makubwa haswa kwenye maswala ya kuundamana na kukusanyika. Waziri amepewe uwezo wa kuongeza vigezo ambayo mtu anatakiwa kuivyipelek polisi kabla ya kufanya mikusanyiko au maandamano.

Na ikitokea mtu hajaridhishwa na maamuzi yaliyo tolewa na polisi anatakiwa akate rufaa kwa waziri wa mambo ya ndani na maamuzi yatakayo tolewa na waziri wa mambo ya ndani ndio maamuzi ya mwisho na wala hayana rufaa.

Pia waziri wa mambo ya ndani amepewa maamlaka ya kuamurukuwa mkusanyiko au maanadamano yeyote yasifuate sharia na taratibu zinahusu mikusanyiko au maandamano na mtu anayeanda maandamo hayo au mkusanyiko huu atakuwa ametenda kosa la jinai

Maoni yangu juu ya maamlaka ya waziri wa mambo ya ndani kuuhusu mikusanyiko na maandamano

Katika mfumo wetu wa Tanzania wazari mambo ya ndani anakuwa ni mwanasiasa wa chama tawala kwaiyo kitendo cha yeye kupewa maamlaka ya kuongeza vigezo anaweza kuongeza vigezo ambavyo vitakuwa vigumu kwa mpinzani wake pia kuamuru mkusanyiko au maandamo ya chama chake au taasisi aliyo na mslahi nayo yafanyike , pia ukiangalia waziri wa mambo ya ndani amepewe maamlaka ya rufani pale inapo tokea mtu hajaridhishwa na maamuzi yaliyo tolewa na chombo cha polisi pia katika hili limetoa mwanya wa ukandamizaji ikitokea mrufani ni mpinzani wa waziri wa mambo ya ndani, yaani kikubwa Zaidi maauuzi ya waziri ndio yatakuwa ya mwisho na wala hayana ruufa, ambapo kwa taswira ya Mahakama inapinga vipengele ambavyo vinapinga jambo kutokufika mahakamani, katika mtizamo wa mahakama inataka ikotokea mtu haridhishwa na maamuzi yaliyo tolewa na chombo chochote cha uongozi kwenda mahakama kuu kuomba marejeo ya uuamuzi.

Mwisho kabisa naona sharia ingaemtaka wazi waziri ni aina gani ya maadamanona mikusanyiko amabayo inaweza isifuate sharia kuliko kumuachia waziri mamlaka makubwa ya kuuamua ni mikusanyiko na maandamano gani yasifuate  taratibu za kisheria, katika utawala wa kisheria unataka kufanya kazi kwa kufata usawa, amapo ukirejere katika ibara ya (13) ibara ndogo ya kwanza ya katiba ya jamhuri wa muungano wa taanzania yam waka 1977 sura ya pili ambayo inamtaka kila mtu kuwa sawa mbele  pasipo kuwepo na ubaguzi wa aina yeyote ile kulindw, kwaiyo mpaka hapo maamlaka aliyo pewa waziri hayako sawa na katiba.

                                     email; jeyma2maduwa@gmail.com 

                                           phone no; (255)  0746804719

                                    

                                     follow me on ;  Facebook@ hd jeyma maduwa

                                                              Instagram@ hd jeyma maduwa

                                                              twitter@  hd jeyma maduwa (rightmndedpason)


Mabadiliko ya Sera na Sheria za Uteuzi wa Viongozi na Wagombea wa Nafasi za Uongozi

Elimu na Uongozi: Hoja ya Mabadiliko ✍️ HD Jeyma Maduwa LL.B. (Hons) Katika zama hizi za maendeleo ya kasi duniani sayansi, teknolojia, uchu...